Kujikaza Kiume.

Ni nani haswa katika familia anayepaswa kusimama na kutetea familia? Appostle Robert Burale hapa kwenye video hii anaeleza kwa mapana na marefu ni kwanini kunapatikana bonde katika uongozi wa familia. Shida haswa iko wapi na jinsi tunaweza kusaidiana kama jamii kuepuka msukosuko huu unaofuata. Sijui wewe uko na wazo gani kuhusiana na swala hili lakini kama utafiti unavyoendelea kuonekana ni kwamba hili ni swala ibuka katika bara Afrika. Wanaume na vijana wanageukia ulevi na mihadarati kuepuka swala hili. Ndio, kama mwaume haufai kulia lakini tufanyeje kuokoa kizazi kijacho? Kwa upande mwingine mashirika yasiyo ya kiserikali yanijaza hela kwa miradi ya kuokoa mtoto wa kike lakini tumesahau ata mtoto wa kiume ni mtoto.