Maskan Flani.

Ewaah! Nimeambiwa na sasa napata kuelewa  kwamba ya Mungu ni mengi na ya kuku ni mayai. Jamaa flani mtaani juzi ametokea sehemu za bara kwao na jogoo mkononi. Kilichotoka kinywani mwake ni kwamba, “huyu jogoo wangu ni wa mbegu peke yake. Ntahakikisha kwamba nimepata wengine kama yeye ndio nimle nyama.” Sisi majirani tulibaki kujionea tu. Yule Chakibanga(Mhusika mkuu) usiku wa kwanza aliota ndoto moja ya maajabu sana. Aliota kwamba yule jogoo anamfukuza kama kikuku kike na kumpanda kana kwamba wanajamiiana. Ebo! mbona mwenzangu akaamka na jasho limemjaa mwilini kama amekutana na simba?

Read more…