Ndawo!

HEKAYA ZA NDAWO

Mashuka Ole Makaptula ndio jina la Kijana fulani wa Kimaasai. Kwao ni kuleee Mphejeto, “kule jua nakuja mafuriko furifuri kama Alasika”, kama anavyojieleza yeye. Mashuka katika umri wake wa ujana ako na mengi ya kujionea kwa ulimwengu wa sasa.Basi siku moja ameenda kutembea jijini Nairobi na katika ile pilkapilka ya kujioneaonea ‘Uptown’ macho yake yakaangukia kuku kwenye kabati za maduka ya vyakula vya haraka. “Shie! Kwani watu ya mujini naanika ndege kwa kabati uchi.”

via Maskan Flani.